Programu Tumizi ya Ms-Word 2019 ni programu ya kukusaidia kuandika vitabu, ripoti, barua na machapisho mbalimbali. Programu hii pia inakuwezasha kuhifandi kumbukumbu mbali mbali ikiwemo mipango ya kibiashara.
Maisha
ya mwanadamu ya sasa yamefungwa katika uandishi. Sehemu kubwa ya kumbukumbu
zinazotomika katika nyanja muhimu sana za maisha zinahifadhiwa katika maandisho.
Hivyo mafanikio yetu hutegemea sana uwezo wetu wa kuandika na kuandika kitalamu
katika utaratibu unaokubalika. Programu tumizi ya Ms-word 2019 inakupa uwezo
mkubwa wa kuandika katika mfumo unakubalika kimataifa. Mafunzo haya yamendaliwa
kwa utalamu wa hali ya juu ili kukupa uwezo wakutumia program hii katika
uandishi wako wa kila siku. Utajifunza kuandika barua, vitabu, ripoti mbali
mbali n.k. Programu hii pia itakupa uzoefu mkubwa wa kujifunza na kutumia
programu zingine za Ms-office kama vile PowerPoint, Excel na Publisher
Walengwa:
Yaliyomo:
Utangulizi (Introduction & Home Tab)
Mandishi (Font)
Kutengeneza Aya (Paragraph formatting).
Orodha (Listing)
Muundo wa mandishi (Text styles)
Kuweka Jedulia (Insert Table )
Kuweka Picha (Insert Picture)
Kuweka Maumbo (Insert Shapes )
Chati Maalumu (Smart Chart)
Grafu (Insert Chart)
Kijajuu na kijachini (Header and Footer)
Kuweka
progamu ( Insert Objects )
Vifaa vya Kufikika kwa Haraka (Text Box, Quick Parts, Drop cap and
Signature Line ).
Namna ya kuchora (Draw )
Muundo (Design)
Mpangilio (Layout)
Marelejeleo
(References)
Kusahihisha (Review)
Muonekano (Views)
Habari:
Mimi ni Mwl Frederick Julius Msangi, ni Madhiri Msadizi chuo Kikuu cha Dodoma na nina udhoefu wa kufundisha katika ngazi hii ya Elimu kwa zaidi ya miaka kumi. Nimebobea katika Maswala ya Elimu ya aulimu, ufundishaji, ujifunzaji na saikolojia. Kwa sehemu, kwa zaidi ya mika nane sasa nimeshiriki katika kufundisha ya elimu ya awali ya TEHEMA (ICT Proficiency Course) kwa wanafunzi wa chuo na washiriki mbali mbali kutoka nje ya chuo.
Nikukaribishe sana katika kujifunza mtandaoni. Mafunzo haya yanatolewa na wabobezi katika maeneo mbali mbali. Niwakaribishe sana katika mafunzo haya, gharama yake ni ndogo sana ukilinganisha na ubora wa mafunzo. Tutakuwa tayari kurejesha fedha kwa ambaye hataridhika na ubora aliyotegemea katika mfunzo haya kama atatoa taarifa hiyo mapema. Piga simu +255655637188 kwa maelezo zaidi. Karibu sana DONE Co LTD.
Write a public review