UTANGULIZI: Mikutano na miadhara imekuwa sehemu kubwa sana ya biashara. Matumizi ya kompyuta yameongezeka sana mashuleni. Ujuzi wa namna ya kuonesha maudhui mbali mbali mbele ya mikusanyiko mikubwa unakuwa siku hadi siku. Programu Tumizi ya MS-Power Point 2019 ni programu maalumu kwa kuandalia onesho (Presentation) kwa hadhira. Kwa kusoma kozi hii utapata ujizi wa kutengeneza wasilisho lako lililobora sana na lakuvutia hadhira.
Walengwa:
Yaliyomo:
1. Utangulizi (Introduction & Home Tab)
2. Kuweka Jeduali kwenye PowerPoint (Insert Table).
3. Kuweka Picha Kwenye PowerPoint (Insert Picture)
4. Kuweka Grafu Kwenye PowerPoint (Insert Chart)
5. Kuweka Video, Suati na Kurekodi (Insert Media).
6.Kutumia Boksi la Maandishi na Kuchapa Hesabu (Insert Objects).
7. Kuweka Grafu Michakato (SmartArt).
8. Muundo wa Slaidi (Slide Design).
9. Uishaji wa Slaidi na Maudhui(Transition and animation).
10. Onesho la Slaidi (Slide Show).
11. Slaidi Mkuu (Slide Master).
Habari:
Mimi ni Mwl Frederick Julius Msangi, ni Madhiri Msadizi chuo Kikuu cha Dodoma na nina udhoefu wa kufundisha katika ngazi hii ya Elimu kwa zaidi ya miaka kumi. Nimebobea katika Maswala ya Elimu ya aulimu, ufundishaji, ujifunzaji na saikolojia. Kwa sehemu, kwa zaidi ya mika nane sasa nimeshiriki katika kufundisha ya elimu ya awali ya TEHEMA (ICT Proficiency Course) kwa wanafunzi wa chuo na washiriki mbali mbali kutoka nje ya chuo.
Nikukaribishe sana katika kujifunza mtandaoni. Mafunzo haya yanatolewa na wabobezi katika maeneo mbali mbali. Niwakaribishe sana katika mafunzo haya, gharama yake ni ndogo sana ukilinganisha na ubora wa mafunzo. Tutakuwa tayari kurejesha fedha kwa ambaye hataridhika na ubora aliyotegemea katika mfunzo haya kama atatoa taarifa hiyo mapema. Piga simu +255655637188 kwa maelezo zaidi. Karibu sana DONE Co LTD.
Write a public review