Karibu katika mafunzo ya namna ya kutumia PHOTOSHOP (PS). PS ni moja kati ya programu (software) ambazo zinaongoza kutumiwa katika tahnia mbalimbali zinazohusisha picha katika kukamilishwa kwake. Na hii ni pamoja na kampuni kubwa duniani zinazojihusisha na filamu zinazotengenezwa kwa teknolojia ya hali ya juu sana yaani sci-fi movies n.k.
Habari:
Naitwa Francis Chebby, ni mmoja kati ya wawezeshaji katika kampuni ya D.O.N.E Co LTD.
Taaluma: Ni mhitimu wa shahada ya awali ya ualimu katika masomo ya sayansi na teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) kutoka chuo kikuu cha Dodoma (UDOM). Lakini pia, ni mhitimu wa digrii ya uzamili katika mambo ya uhifadhi wa bioanuwai (viumbe hai na mazingira) kutoka chuo kikuu cha Dodoma (UDOM).
Uzoefu: Mbali na kuhusika katika uwezeshaji na usimamizi wa shughuli mbalimbali za kitaaluma ndani na nje ya chuo kikuu cha Dodoma, kwa sehemu nimekuwa mmoja kati ya wafundishaji wa mafunzo ya awali ya TEHAMA (ICT Proficiency Course) kwa wanafunzi wa chuo kikuu cha Dodoma nawashiriki mbali mbali kutoka nje ya chuo kwa zaidi ya miaka 3. Uzoefu huu umekuwa nguzo na muhimili mkubwa katika kukuza uwezo na kuboresha namna ya kuandaa mafunzo mbalimbali kwa njia rahisi, ubora mkubwa na kueleweka mno kwa mfuatiliaji husika.
Maoni yangu: Katika kipindi ambacho TEHAMA ina umuhimu mkubwa sana katika masuala ya kijamii hasa kukuza kipato, ni jukumu letu kuhakikisha atupitwi na fursa mbali mbali zenye uhitaji wa teknolojia hii. Kwa kulitambua hilo, sisi kama wawezeshaji wenye taaluma stahiki kutoka kampuni ya D.O.N.E co LTD, tunayofuraha kuwafungulia ulimwengu wa kutumia TEHAMA kukuletea mafunzo mbali mbali yahusuyo elimu, michezo, ujasiriamali, afya ya mwili na akili, ubunifu na mambo mengine mengi kwa njia rahisi na masharti nafuu sana. Huu ndio wakati sahihi. Tumia fursa.
Mawasiliano:
D.O.N.E Coordinator: +255 655 637 188
Mawasiliano yangu: +255 769 535 944
Write a public review