Mr. Francis Chebby

Show full biography

Habari:

Naitwa Francis Chebby, ni mmoja kati ya wawezeshaji katika kampuni ya D.O.N.E Co LTD.


Taaluma: Ni mhitimu wa shahada ya awali ya ualimu katika masomo ya sayansi na teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) kutoka chuo kikuu cha Dodoma (UDOM). Lakini pia, ni mhitimu wa digrii ya uzamili katika mambo ya uhifadhi wa bioanuwai (viumbe hai na mazingira) kutoka chuo kikuu cha Dodoma (UDOM).


Uzoefu: Mbali na kuhusika katika uwezeshaji na usimamizi wa shughuli mbalimbali za kitaaluma ndani na nje ya chuo kikuu cha Dodoma, kwa sehemu nimekuwa mmoja kati ya wafundishaji wa mafunzo ya awali ya TEHAMA (ICT Proficiency Course) kwa wanafunzi wa chuo kikuu cha Dodoma nawashiriki mbali mbali kutoka nje ya chuo kwa zaidi ya miaka 3. Uzoefu huu umekuwa nguzo na muhimili mkubwa katika kukuza uwezo na kuboresha namna ya kuandaa mafunzo mbalimbali kwa njia rahisi, ubora mkubwa na kueleweka mno kwa mfuatiliaji husika.


Maoni yangu: Katika kipindi ambacho TEHAMA ina umuhimu mkubwa sana katika masuala ya kijamii hasa kukuza kipato, ni jukumu letu kuhakikisha atupitwi na fursa mbali mbali zenye uhitaji wa teknolojia hii. Kwa kulitambua hilo, sisi kama wawezeshaji wenye taaluma stahiki kutoka kampuni ya D.O.N.E co LTD, tunayofuraha kuwafungulia ulimwengu wa kutumia TEHAMA kukuletea mafunzo mbali mbali yahusuyo elimu, michezo, ujasiriamali, afya ya mwili na akili, ubunifu na mambo mengine mengi kwa njia rahisi na masharti nafuu sana. Huu ndio wakati sahihi. Tumia fursa.


Mawasiliano:

D.O.N.E Coordinator: +255 655 637 188                                                       

Mawasiliano yangu: +255 769 535 944

                  

  • Total student
    4
  • Courses
    2
  • Reviews
    0